Ikiwa na ari, nguvu na kujaa hamasa na matumaini ya kushinda, timu ya mpira wa miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kesho Jumamosi Agosti 6, 2016 itaingia Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Magharibi mwa Mji wa Johannesburg, Afrika Kusini kucheza na wenyeji katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika Madagascar hapo mwakani.

“Tutaifunga Afrika Kusini hapa kwao,” ni maneno ya Mchawi Mweusi - Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, alipozungumzia mchezo huo utakaoanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huko Tanzania itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya Moroka Swallows ambayo kwa sasa imeshuka daraja hadi la pili.

Afrika Kusini ambayo Serengeti Boys inacheza nayo kesho ni mtihani wa kwanza kati ya miwili kabla ya kutinga Madagacar. Mchezo wa kwanza unafanyika hapa Afrika Kusini, kabla ya kurudiana Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi-nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Mchawi Mweusi ambaye jina lake halisi ni Bakari Nyundo Shime, amesema: “Kwa jinsi tulivyojiandaa. Sina wasiwasi na timu yangu.”

Shime amesisistiza: “Najua Afrika Kusini watataka kutumbia mbinu za nyumbani. Lakini sina wasiwasi. Nimelenga kushinda michezo yote iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu kwenda Madagascar tu kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii niipeleke Kombe la Dunia.”

Shime ambaye alianza na timu hiyo mwaka mmoja uliopita, amerudia maneno yake: “Sioni kama itakuwa kikwazo kuifanikisha kufika fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu atunyooshee mkono wake, nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu hii, lakini pia wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au kuchagua mtu anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote.”

Shime alishukuru mipango na ahadi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kugharamia kambi ya siku 10 iliyoyofanyika Madagascar akisema: “Ilikuwsa ni kambi bora. Kwa sasa kikosi changu kinahitaji kulipam deni la Watanzania na ahadi ya Rais Malinzi.”

Kikosi tarajiwa kesho ni Ramadhani Awm Kabwili atakayecheza golini, Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Vitalis Nkosi, Dickson Nickson Job, Shaban Zuberi Ada, Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Mohammed Abdallah Rashid Ibrahim Abdallah Ali na  Syprian Benedictor Mtesigwa.

Ili kufika hapo, Serengeti iliifunga Shelisheli jumla ya mabao 9-0 katika mechi mbili za Tanzania na Shelisheli.

Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...