Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mijini kwa Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa gari moshi litalofanya safari zake kuanzia Stesheni ya Dar es salaam hadi Pugu. Amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45.
Amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapungaza kama sio kumaliza kabisa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. 

 Profesa Mbarawa amesema kuwa katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo.
Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli.
Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali.
Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kwa usafiri huo wameanza kutokana na nguvu ya serikali kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Safari inaendelea.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi usibane:

    JamiiForums watwambie kwa nini (significance and rationale) ya kuanzia na Jimbo la Bukobba Mjini?

    Je, watafungua nafasi hiyo kwa kila jimbo la uchaguzi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...