Baadhiya Bodaboda za washiriki zikiwa zimepaki bila kufanya kazi ya kubeba abiria ambapo wamiliki walikuwa kwenye mafunzo

Na Mathias Canal, Singida

Serikali imeeleza kuwa ipo tayari kuchukiwa na wananchi wavivu wasiotaka kujishughulisha na Ujasiriamali, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara ili kukuza pato la kaya zao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kufunga mafunzo ya usalama Barabarani kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi yaliyohusisha Kata ya Issuna na na Kata ya Mkiwa na kufanyika JMC Hotel Kijijini Issuna B.

Katika mafunzo hayo yaliyochukua siku sita yamewakutanisha pamoja waendesha Bodaboda 84 ambao wamefundishwa Alama na sheria zote za usalama Barabarani, Upatikanaji wa leseni, Faida za kulipa kodi na somo la ujasiriamali, Polisi jamii, Ulinzi shirikishi na elimu juu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo ya usalama barabarani.

Akiwahutubia wananchi hao Mtaturu amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ajira ya pikipiki kwani kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza uhalifu na kuandaa ajira kwa vijana wengi nchini hivyo kuachana na kujihusisha na mambo yasiyo na tija kwa jamii ikiwemo kushinda vijiweni.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la APEC yatasaidia kupunguza ajali za pikipiki zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya waendesha pikipiki katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.

Dc Mtaturu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha madereva Bodaboda waliokwepa mafunzo ya awamu hii wanasajiliwa ili wahudhurie mafunzo yatakayorudiwa kwa awamu ya pili kwa Wilaya nzima, hivyo kwa wale ambao hawatapata mafunzo hawataruhusiwa kuendesha pikipiki zao ili kuepusha ajali mpaka pale watakapopata mafunzo.
Dc Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa APEC Respicius Timanywa zawadi ya kuku iliyotolewa na wahitimu wa mafunzo hayo

“Dereva bila elimu ni sawa na bunduki bila risasi, hivyo nakuagiza mkuu wa Polisi kutowakamata kwa kosa la kutokuwa na leseni angalau kwa kipindi cha miezi miwili wakati wanafuatilia leseni zao”  Alisema Mtaturu

Akizungumzia kuhusu alama za barabarani Mtaturu alisema kuwa tayari ameshamwagiza Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri kufanya mawasiliano na wakala wa barabara katika maeneo yote ambapo alama za barabarani hazipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...