THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERIKALI KURASIMISHA KAZI ZA SANAA NCHINI


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga gitaa na kuimba wakati wa uzinduzi wa shindano la Club Raha Leo msimu wa tatu katika ukumbi wa Club 71 Kibo Complex Tegeta Jijini Dar es Salaam Agosti 7,2016.









Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imedhamiria kurasimisha kazi ya sanaa kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizundua msimu wa tatu wa kipindi cha televisheni cha kusaka vipaji vya wasanii chipukizi cha Club Raha Leo Show na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wadau wa sanaa na wasanii ili kufanikisha azma ya serikali ya kurasimisha sekta hiyo kuwa rasmi kama shughuli ya kiuchumi.

“Tutashirikiana na nyinyi katika kuiendeleza sekta ya sanaa nchini ili kuwezesha vijana wengi wenye vipaji kuweza kujiajiri na kuajiri wengine kupitia kazi zao za sanaa” alisema Mhe. Nape.

Mhe. Nape Moses Nnauye amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano mbalimbali ya kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kuweza kufikia malengo ya kuendeleza sekta ya sanaa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba amesema kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litaendelea kushirikiana na wadau wa sanaa nchini kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii mbalimbali ili kuwezesha sanaa kuwa ajira rasmi katika kuinua kipato cha msanii na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Naye Mratibu wa Club Raha Leo Show Bibi. Susan Mungi amesisitiza wasanii kuheshimu kazi zao na kuzifanya kwa ustadi mkubwa kwani ndio nyezo muhimu katika kuendeleza kazi ya sanaa nchini kwa kuifanya kuwa kazi mojawapo ya kiuchumi.

Club Raha Leo Show ilianzishwa kama Kipindi cha redio kilichorushwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuwa shindano kubwa Tanzania la kusaka, kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wanaochipukia nchini, na huu ni msimu wa tatu wa shindano hilo.