Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso
Puente, wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kushoto), akisaini
Kitabu cha Wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (Kulia), alipomtembelea Waziri na kufanya naye
mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika
uwekezaji kwenye sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto),
akimsikiliza kwa makini Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso
Puente (Kulia), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Ofisini kwake
jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu
masuala ya uwekezaji katika sekta za nishati na madini. Wengine pichani
ni Maafisa wa Wizara waliohudhuria mkutano huo.
Na Veronica Simba
Serikali ya Brazil imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini
hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia maji na mabaki ya miwa.
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Brazil nchini
Tanzania, Carlos Alfonso Puente, alipomtembelea Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo
naye.
Balozi Puente alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi yake inao ujuzi na
uzoefu wa kutosha katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo
mbalimbali hususan maji.
Alisema, Brazil ingependa kuchangia kufanikisha azma ya Rais John
Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Kutekeleza mchakato wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda, unahitaji
umeme mwingi unaotokana na vyanzo mbalimbali. Ni bahati nzuri kwamba
Tanzania inazo njia za kufanikisha azma hiyo,” alisema.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Kwa kweli lazima niseme hili. Mhe Muhongo anautaratibu fulani unafaa kuingwa. Miaka yote alokuwa Waziri anapenda kufanya mikutano na wageni inayowajumuisha watendaji wake. Hili linsaidia kuwajenga na pia ni msingi mzuri wa uwazi. Nalisema hili kwani yule aliyekuwa Waziri wa Maliasili awamu iliyopita Mhe Nyalandu yeye alikuwa mara kwa mara anakutana na wageni bila hata kuwashirikisha watendaji wake wakuu. Ulikuwa unawaona wamekaa meza za mbali pembezoni wakati Mhe Waziri pekee anakutana na wageni kutoka nje. Hili nimelishuhudia ndani na nje ya nchi. Hata kuna wakati Katibu Mkuu wake naye hakuhusishwa mpaka wageni wakauliza kwanini hashiriki? Utakuta yupo peke yake kazungukwa na wageni na watendaji wake wanasubiri awataarifu kilichojiri!!! Lazima Tanzania tubadilike. Akina Muhongo wanamsaidia Magufuli kufanya hivyo. They deserve our support.
ReplyDelete