Na Frank Shija, MAELEZO
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vitakavyo jikita katika fani za Usafirishaji vitakavyojengwa Barani Afrika kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho alipokutana na Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Bwana Lin Zhiyong wakati wa ziara ya kufanya tathmini juu ya uwezo wa NIT katika utoaji wa elimu ya Usafirishaji na namna ya kuweza kukisaidia chuo hicho.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo amemuhakikishia Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa NIT iko imara na inayo mipango kabaambe kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho utakao enda sambamba na kuongezeka kwa Programs zitakazokuwa zikifundishwa.
“Kutokana na urafiki wa muda mrefu tulionao baina yetu na China ni imani yangu kuwa Chuo hiki kitakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji vitakavyojengwa kwa masaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China barani Afrika kama ambavyo Rais wan chi hiyo alivyo dhamiria wakti wa mkutano huko Afrika ya Kusini” Alisema Dkt. Chamuriho.
Ni dhahiri kuwa wataalamu wa masuala ya usafirishaji wanatakiwa kwa wingi kwani ukuaji wa Sekta hiyo unaenda kwa kasi hali kadhali Jiografia ya nchi yetu inatoa fusra kwa Tanzania kujenga miundombinu ya usafirishaji kama vile Barabara na miundombinu ya Reli, Viwanja vya Ndege ili kuunganisha na Bandari.
Mpango huo umekuja katika wakati muafaka kwani utasaidia kuongeza idadi ya waataalam katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa wanafunzi wengi zaidi watajiunga na masomo mbalimbali yatakayofundishwa katika chuo hicho kitakapo kamilika.
Mhandisi Profesa Zacharia Mganilwa ni Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji, anasema kuwa wao kama uongozi wa chuo wanao mpango mahususi wa kufanya maboresho makubwa ya Chuo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji halisi ya Sekta ya usafirishaji hapa nchini kwa sasa.
“Sisi kama Taasisi tumejipanga kuhakikisha tunafanya maboresho ya Chuo chetu ili kiendane na hali halisi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji hapa nchini, katika mpango huo tumenuia kuanzisha Shule tano zitakazo jikita katika nyanja za Shule ya Uhandisi na Teknolojia, Shule ya Teknolojia ya Anga, Shule ya Usafirishaji na Logistic,Shule ya Elimu, Hisabati na Kompyuta na Shule ya Biashara NIT”. Mhandisi Mganilwa
Aliongeza kuwa kutokana na mpango huo NIT inalo maeneo yakutosha na kukidhi mahitaji ya utekelezaji wa mpango huo kwani ina jumla ya ekari 46 katika eneo la sasa ambapo kuna ardhi ekari 46 ambapo kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndiyo iliyotumika hadi sasa, pia chuo kimefanya utaratibu wa kupata eneo jingine la ekari 1600 katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
kizungumza wakati wa ziara hiyo ya kufanya tathmini ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong ameonyesha imani kwa Chuo hicho na kuahidi kusaidia katika kuhakikisha kinakuwa miongoni mwa Vyuo hivyo Vitano vilivyoahidiwa na Rais wao.
Aliongeza kuwa kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itakuwa nchi ya uchumi wa kati.
“Nimeshawishika na niliyojionea hapa naweza kusema Serikali yetu itakuwa tayari kusaidia program mbalimbali zilizopo hapa na kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo nawahakikishia kuwa  NIT itakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kama ambavyo Rais wetu alivyo ahidi wakati wa Mkutano Jijini Johannesburg, Afrika Kusini”.Alisema Zhiyong.
Zhiyong aliongeza kuwa ujenzi huo wa Vyuo hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Ziara hiyo ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya program zinazofundishwa, rasilimali watu na miundombinu kwa maana ya eneo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt. Leonard Chiriho  akizungumza na wawakilishi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walipotembelea Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Wawakilishi hao wametembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika.    Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi. Profesa. Zacharia Mganilwa, Katibu wa Tatu Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Sun Chengfeng, Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong na Mkurugenzi wa Huduma za Uasafirishaji kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Aron Johnson Kisaka.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt. Leonard Chiriho akimzungusha Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong (katikati) alipotembelea Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi huyo alitembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa.
Picha na Frank Shija, MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...