Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar pamoja imewahasa wazazi nchini kutoa uhuru kwa watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu ili kuifikisha nchi katika Mashindano ya Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Hassan Mitawi alipokuwa akifungua mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Alisema bila ya michezo Zanzibar haiwezi kujulikana hivyo ni vyema kwa wazazi na walezi kuwapa motisha watoto wao wa kike kushiriki katika michezo hasa mpira wa miguu.

Alisema mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wenye kutoa ajira kama ilivyo kwa wanaume lakini tabia ya baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao wa kike kujiingiza katika soka kunawakosesha fursa zinazotokana na mpira ikiwemo afya bora, ajira pamoja na kuchangia katika kukuza soka la wanawake nchini.

Mitawi alisema watu wanazaliwa na vipaji na vipaji hivyo vinapaswa kuendelezwa hasa kwa upande wa Zanzibar wanawake washirikiane kudumisha michezo.

Aidha aliishukuru Airtel kuzidi kukuza na kusaidia michezo nchini na kuwataka kuendelea kuwekeza katika michezo hususani soka la wanawake.

Awali Mwenyekiti wa soka la wanawake Hatima Mwalimu alisema mashindano hayo yatasaidia kuinua vipaji vitakavyoisaidia Zanzibar kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Nae Meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Muhidin Mikadadi alisema “Tunajisikia fahari kusaidia mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hapa nchini na tumejipanga kuibua vipaji vya vijana kupitia program hii. Tunafurahi kuona vijana wengi wanajitokeza kushiriki mashindano hayo na tunawashukuru ZFA na Wizara ya Michezo kuwaunga mkono katika kusaidia na kukuza michezo nchini”.

Huu ni msimu wa sita kwa mashindano ya Airtel Rising Star nchini kwa mwaka humu Zanzibar impeta nafasi ya kushiriki, jumla ya timu sita zinashiriki katika mashindano haya ni pamoja na Mwenge kutoka Wilaya ya Kusini, Kidimni Kutoka Wilaya ya Kati,New Generation Kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi, Jumbi Women kutoka Wilaya ya Kati na Bungi Sisters kutoka Wilaya ya Kati.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamanduni na Michezo Zanzibar Hassan Mitawi akikangua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Ijumaa 5 Agosti 2016.
Mchezaji wa Bungi Sister FC Agatha Peter (nyekundu) akichuana na beki wa Jumbi Woman Fighter Arafa Mbaraka wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huwa kuna ule msemo maarufu usemao..."Zanzibar ni njema atakae na aje." Ingekuwa michezo kama vile nage, hadimfundo, kobole na mingineyo nakhisi wasingesubiri hata upatu upigwe, ila hili la mpira wa miguu kwa malezi, mila, desturi, itikadi na maadili khususan ya mila na kiimani, nadhani kwa leo na kesho kwa wazanzibari khasa halisi mpira wa miguu kwa mtoto wa kike, nakhisi litachukuwa muda mpaka kuhamasika. Hayo ni mawazo yangu na the way nnavyoyafaham mazingira ya malezi ya mtoto wa kike kwa uelewa wangu kiasi kwa huko visiwani. Ila pongezi kwa Wizara husika kwa kulihamasisha hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...