Mwenyekiti
wa Bodi wa Shule za Feza, Habib Miradj akizungumza na waandishi wa
habari juu kuhusiana na taarifa zinazozagaa za kufungwa kwa shule za
Feza leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa shule wa Feza, kadri
dalcicea.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHULE
za Feza nchini hazitafungwa kutokana na shule hizo zimesajiliwa kwa
mujibu wa sheria za nchi hivyo ikibidi kufanya hivyo sheria zitatumika
zilezizle zilizofanya shule hizo zisajiliwe.
Hayo
ameyasema leo Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Feza, Habib Miradj wakati
alipokutana na waandishi wa habari leo juu ya kuzagaa kwa taarifa katika
mitandao si michuzi blog juu ya shule za fedha kufungwa, amesema kuwa
taarifa hizo hazina ukweli na kuwataka wazazi kuendelea kuwaunga mkono
katika kusukuma gurudumu la elimu.
Amesema
Feza imekuwa ikijulikana kimataifa kwa kufanya vizuri na kuweza kupata
tuzo mbalimbali katika utoaji wa elimu ikiwa na wanafunzi wanaokwenda
katika vyuo vya ndani ya nje wamekuwa wakipata ufaulu wa juu.
Miradj
amesema kuwa wakaguzi shule wamekuwa wakienda na kuwashauri vitu
mbalimbali hivyo hata kufungwa kwa sheria zitatumika lakini suala hilo
halitegemei kutokea katika shule zetu za feza kutokana na hadhi ambayo
imefikia katika utoaji wa elimu.
Aidha
amesema kuwa Feza inazidi kujiimarisha katika utoaji wa elimu na
kuongeza kuwa mpango wao kuhakikisha shule zinaongezeka katika baadhi ya
maeneo kutokana na mahitaji ya elimu nchini.
Amesema
historia ya Feza imetokana na juhudi za serikali ya kutaka uwekezaji
wa shule ufanywe nchini baada kuonekana kufanya vizuri nchini Uturuki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...