THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SHULE ZA FEZA HAZITAFUNGWA


UONGOZI wa  Shule za Feza nchini umeibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii,  kuwa wao  hawana uhusiano na  Fethullah Gulen wala serikali ya Uturuki  kwa vile   hawajawahi kupokea misaada toka pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.
Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule za Feza  zipo hatarini kufungwa kwa madai kuwa  mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji amesema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama asasi  zingine zilizosajiliwa kishera na serikali, hivyo ni mali ya watanzania.
“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda  cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania  na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.
Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.
Aliongeza kuwa  huo ni uwekezaji  wenye mchango katika kukuza pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.
Alisema  wanatoa  wito kwa wazazi  kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo  kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.