SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imesema imeanza mchakato wa kushirikisha wananchi kuchangia maoni yao juu ya kubadilisha kwa sheria ya ndoa ya sasa inayoonekana kuwa kandamizi kwa wanawake; https://youtu.be/3rIwDf-689o
SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa, ametoa siku 14 kwa mkandarasi anayejenga barabara wilayani Sumbawanga kurudisha vifaa na kuendelea na kazi; https://youtu.be/cR41cwg4Lbo
SIMU.TV: Wakazi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa agizo la kuanza kufanya kazi kwa soko lao; https://youtu.be/thcK5duLqRI
SIMU.TV: Waziri wa Maliasili na utalii Prof Jumanne Maghembe, amezindua bodi ya wakurugenzi ya bodi ya utalii nchini na kuitaka bodi hiyo kuongeza idadi ya watalii;https://youtu.be/EnYfivzMBOs
SIMU.TV: Shirika la umoja wa mataifa lam maendeleo na bisahara UNCTAD, limeuingiza mkoa wa Njombe katika mafunzo ya kufuga ng’ombe kitaalamu;https://youtu.be/qT9T_lYcSnE
SIMU.TV: Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imetoa agizo kwa watu wote waliovamia maeneo ya wazi waondoke mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.https://youtu.be/4rXX6j9lS-Q
SIMU.TV: Waziri wa katiba na sheria Dr. Haryson Mwakyembe amesema serikali imefanya jitihada kubwa za kuhakikisha inalinda uhuru na haki za mwanamke.https://youtu.be/3oX9dpXzccw
SIMU.TV: Serikali imepiga marufuku tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyogaiwa kufugia kuku au kuvitumia kupandia miti. https://youtu.be/-5bNXAx2Pc4
SIMU.TV: Jumla ya hati laki tatu zinatanatarajiwa kutolewa kwa wakazi wa Dar es Salaam baada ya zoezi la urasimishaji wa makazi holela kukamilika. https://youtu.be/OX0c-GC84Yw
SIMU.TV: Jumla ya watu 93 kati ya watu 1453 waliojitokeza kuchangia damu katika mkoa wa Tanga wamebainika kuwa na homa ya ini. https://youtu.be/xPQIb_-d7PY
SIMU.TV: Wachinjaji wa ng’ombe na mbuzi katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi kutokana na kupandishiwa ushuru.https://youtu.be/M_V8l5eUsXg
SIMU.TV: Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imesogeza mbele kesi inayomkabili mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lisu ya kutoa maneno ya uchochezi.https://youtu.be/1cpA8TL8YJY
SIMU.TV: Serikali imepiga marufuku kilimo cha mkataba kilichokuwa kikimnyonya mkulima kutokana na mnunuzi kujipangia bei ya mazao. https://youtu.be/uihwW2qN_NU
SIMU.TV: Serikali imeishauri mifuko ya hifadhi za jamii hapa nchini kutumia huduma za utuzaji wa dhamana za uwekezaji ili kuwezesha fedha za wateja wao kuwa salama zaidi.https://youtu.be/ukt9omDKAhs
SIMU.TV: Baadhi ya taasisi za fedha zimeanza kuitikia wito wa serikali wa kushusha riba za mikopo ili kuwapa fursa watanzania wengi kupata mikopo.https://youtu.be/yQZXb5osMUE
SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu TFF limesema halitatoa leseni kwa mchezaji ambaye timu yake haikuwasilisha mkataba wake kwa TFF. https://youtu.be/d8gFwFIfYwU
SIMU.TV: Mwanachama wa klabu ya Simba Mohamed Dewj ameikabidhi klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni mia kwa ajili ya usajili wa wachezaji. https://youtu.be/JUJ3oCO9Zv4
SIMU.TV: Takribani wasanii 10 wa filamu na muziki nchini wanatarajia kunufaika kwa kujiingizia kipato kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kuanzishwa kwa b nary itakayosimamia urushwaji wa matangazo kwa mitandao yote ya kijamii.https://youtu.be/99gmONc9-vE
SIMU.TV: Wanafunzi wa kike wametakiwa kutojiweka kando bali washiriki katika michezo ili kuweza kuonesha vipaji vyao na kuviendeleza. https://youtu.be/hLY42CzFuw4
SIMU.TV: Manchester city imekamilisha usajili wa kiungo chipukizi Leroy kwa kiasi cha pound milioni 35 akitokea Schalke 04. https://youtu.be/Ap9iBI5jMhY
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...