THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kua waalimu wote wanatarajia kusafiri bure kwenye usafiri wa treni ya abiri jijini Dar es salaam.https://youtu.be/uuHgPBv1-cU

SIMU.TV: Taasisi ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela inatarajia kuanza mradi wa kusafisha maji ya bwawa la Nadosaito wilayani Monduli ili wananchi wapate maji safi.https://youtu.be/jiqNgrflcxw

SIMU.TV: Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wa kufuta kosa la utakatishaji wa fedha kwenye kesi ya Hary Kitilya na wenzake. https://youtu.be/zB2tU_YAJbs

SIMU.TV: Baadhi ya shule mkoani Manyara zinaelezwa kukabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayowafanya wanafunzi kusomea kwenye bweni katika shule ya  sekondari Engeno wilayani Simanjiro. https://youtu.be/-QEutPcpC84

SIMU.TV: Moto umeteketeza baa maarufu ya Carebean iliopo eneo la Sinza jijini Dar es Salaam na kusababisha uharibifu mkubwa. https://youtu.be/mLm4JR740zA

SIMU.TV: Shule ya msingi Msufini iliopo Mbagala jijini Dar es Salaam inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa kutokana na kuwa na wanafunzi wengi.https://youtu.be/qxC_K5GadzM

SIMU.TV: Uongozi wa bodi ya utalii nchini TTB umetembelea kampuni ya habari ya Africa Media Group ili kuangalia namna ya kushirikiana katika kukuza utalii wa ndani.https://youtu.be/maeWbvvau0s

SIMU.TV: Shirika la viwango nchini TBS limeanza mazungumzo ya uboreshaji wa matakwa ya viwango na wadau ili kuwa na bidhaa zenye viwango vinavyokubalika.https://youtu.be/mqf7_v5hyz0

SIMU.TV: TBS imekifunga kiwanda cha uzalishaji wa mikate cha Herry Bakery kutokana na kuzalisha bidhaa bila kuwa na nembo ya ubora. https://youtu.be/4D3lL1jx-jY

SIMU.TV: Ligi ya taifa ya mpira wa wavu inatarajiwa kuanza tarehe kumi na nane mwezi huu wilayani Kibaha mkoani  Pwani na itashirikisha timu kutoka mikoa mbalimbali.https://youtu.be/jb61SteedIE

SIMU.TV: Mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na mbunge wa jimbo la Songea mjini yamehitimishwa kwa washindi kukabidhiwa zawadi zao.https://youtu.be/rYO_tKZOXF8

SIMU.TV: Meneja wa klabu ya Arsenal amesema hatma yake ya kuendelea kuifundisha klabu hiyo itategemea matokeo ya klabu hiyo msimu huu wa ligi kuu Uingereza.https://youtu.be/d6DNxIjl74w