THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Spika wa baraza la wawakilishi zanzibar aongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 47 ya Nchi za Jumuiya za Madola kanda ya Africa.

 Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Tanguu Zanzibar Mhe. simai Mohamed Said akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Mussa Hassan Zungu na Mh Raphael Chegeni huko Mauritius katika mkutano wa 47 ya Nchi za Jumuiya za Madola kanda ya Africa.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh Zubeir Maulid Zanzibar akitembelea ofisi ya Meya wa Mji Mkuu wa Mauritius Port Louis Mstahiki Oumar Kholeegan na kumualika kuja kuona mji wa Zanzibar ambao una sura ya mfanano na historia kama yao. Kulia ya Meya ni Mh Simai Mohammed Said, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Jimbo la Tunguu Zanzibar.
 Mh Zubeir Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi akiambatana na wageni mbali mbali pamoja Mh Simai 'Mpakabas' katika kutembelea kiwanda cha kufulia umeme kwa kutumia mabaki ya miwa.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh Zubeir Maulid, Mhe. simai Mohamed Said pamoja na Mhe Maria Ndilla Kangoye Mbunge wa Jamhuri ya Muungano katika ziara ya matembezi ya kuutembea mji mkuu wa Mauritius, Port Loius.