THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

STDFAA wamuomba Nape kuharakisha Sera ya filamu.

 Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni wasanii wa chama cha Waigizaji cha Mkoa wa Kinondoni (STDFAA).

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
CHAMA cha Waigizaji cha Mkoa wa Kinondoni (STDFAA) wamemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye kuiharakisha Sera ya filamu ili iwasaidie katika mambo mbalimbali hususani ya kisheria.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika tasnia ya filamu nchini.

Makatu amesema kuwa Sheria ya Filamu ni muhimu katika tasnia hiyo hivyo ikiharakishwa itasaidia wadau wa tasnia hiyo kufanya kazi kwa uwazi na usalama wa hali ya juu kwa kuwa watakua wanalindwa na sheria.

“Tunamuomba Waziri wetu Mhe. Nape atuharakishie Sera ya Filamu kwa sababu sheria hiyo itatusaidia kuoanisha mambo mbalimbali ya kisheria kuanzia kwenye uandaaji wa kazi zetu hivyo, kupelekea kufanya kazi kwa  ufanisi na kutoa kazi bora zaidi”. Alisema Makatu.

Ameongeza kuwa sheria hiyo pia itawasaidia katika suala zima la Haki miliki na Haki shiriki, malipo stahiki kwa kila kazi, masoko, madaraja ya waigizaji na wadau wote wa tasnia ya filamu pamoja na ulazima wa kila msanii kujiunga katika vyama husika vitakavyowasaidia katika mambo mbalimbali.

Aidha, Katibu huyo ameiomba Serikali kuwekeza kwenye sanaa ili kuwawezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuchangia katika Pato la Taifa pia amemuomba Mhe.Nape kuwatafutia eneo maalum la ardhi ambalo litawasaidia katika kufanyia shuhuli zao za kurekodi filamu.

Ametoa rai kwa wasanii kujiunga katika vyama mbalimbali vinavyowahusu ili kuleta umoja, mshikamano na tija katika kazi za sanaa,amesisitiza wasanii kujiunga na Bima za Afya.

Naye Mdhamini wa Chama hicho, Ahmed Olotu amewaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuwasaidia wasanii kupambana na wauzaji  wa filamu feki kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya wasanii na kupunguza pato la Taifa.