Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano. 
“Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa-
Deogratius Munishi – Young Africans, Aishi Manula – Azam FC
 Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans, Vicent Andrew - Young Africans, Mwinyi Haji - Young Africans,Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC,David Mwantika - Azam FC
 Viungo
Himid Mao - Azam FC, Shiza Kichuya – Simba SC, Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar, Jonas Mkude – Simba SC, Muzamiru Yassin – Simba SC, Juma Mahadhi - Young Africans , Farid Mussa Tenerif ya Hispania
 Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans, Jamal Mnyate – Simba SC, Ibrahim Ajib – Simba SC , John Bocco - Azam F, Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...