Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA anasikitika kutangaza kifo cha mmoja wa watumishi wa Mamlaka, Bwana James Emmanuel Kitainda (pichani) , kilichotokea siku ya Jumatano, tarehe 10 Agosti, 2016 jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda. 

Bwana Kitainda alijiunga na PPRA kama mtaalamu wa manunuzi mwezi Novemba, 2008, na alikuwa akifanya kazi kwenye Idara ya Ufuatiliaji na Ukidhi. 

Kabla ya kujiunga na PPRA, Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Fedha na Mipango katika iliyokuwa Halmashauri Kuu ya Zabuni, kama afisa ugavi. 

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele Jumamosi tarehe 13 Agosti, 2016 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. 



Mwenyezi Mungu ailaze roho ya 
Marehemu mahala pema peponi. Amina. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. pumzika kwa amani babu!

    ReplyDelete
  2. Hakika Kila Nafsi itaonja Mauti,Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea kwa wakati uliopangwa...! Pumzika kwa amani James Kitainda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...