Na Selemani Semunyu JWTZ 

Timu ya Mpira wa Pete ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imedhihirisha Ubabe wake katika mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Rwanda RDF kwa Magoli 56-13 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na Timu zote tangu kuanza Mashindano hayo. 

Tangu Mwanzo wa Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Rwanda walionekana kuzidiwa na kiwango kilichoonyeshwa na Tanzania kupitia Nyota wake Mwanaidi Hassan aliyefunga 37 na Nasra Suleiman aliyefunga 19 waliokuwa mwiba kwa Timu ya Rwanda kutokana na kupachika magoli kila wapatapo mpira. 

Tanzania iliweza kumiliki vipindi vyote vine vya mchezo huku Rwanda wakionekana kutoelewana kutokana na idadi ya magoli waliokuwa wakifungwa tangu Robo ya Kwanza mbayo ilimalizika kwa Tanzania kuongoza kwa 13-2 huku Robo ya pili 32-6 na Robo ya tatu 42-10.
Kwa upande wake Mchezaji Nasra Suleiman alisema mbali na kupata ushindi huo lakini hawatobweteka kwani wanawasubiri Kenya ili kutangaza Ubingwa kwa kushinda Michezo yote. 

Kwa upande mwingine Tim u ya Mpira wa Miguu ya Tanzania wameinyamazisha Timu ya Jeshi ya Kenya baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
Katika Mchezo huo Kenya Ndio walianza kupata bao Muda mchache kabla kwenda mapumziko katika Dakika ya 42 kupitia kwa mchezaji wake Private Peter Onyango kabla ya Dakika tatu Baadae Private Prosper Mkwama kusawazisha bao na kwenda mapumziko wakiwa Sare.; 

Kipindi cha Pili kilianza huku Timu zote zikifanya mabadiliko na kosa kosa ya magoli kwa Nyakati tofauti lakini Mnamo dakika ya 77 Private Abdulrahman Musa akaiandikia Tanzania bao la Pili na la ushindi.
Kufuiatia matokeo hayo sasa Tanzania wamebakiza Mchezo mmoja na Rwanda utakaopigwa siku ya ufungaji Agosti 17 katika Uwanja wa Amahoro huku Timu ya mpira wa Pete wanatarajia kukutana na Kenya Agosti 14. 
 
Mlinzi wa Timu ya Mpira wa Pete wa Tanzania Joyce Kaira (GK) akiwa katika hekaheka za kuzuia Wachezaji wa Rwanda Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13
Kocha wa Timu ya Tanzania kwa Mpira wa Pete Argentina Daudi akitoa maelekezo kwa Wachezaji wake katika muda wa mapunziko katika mchezo baina yao na Rwanda uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali ambapo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
Nyota Chipukizi wa Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( Mwenye Mpira)akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika  mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Africa Mashariki wenzao wanatesa Olympic! Tanzania Bawana!! A country of low expectations!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...