Baraza la Ushauri kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania ( TCRA CCC) leo limekabidhi vyeti na zawadi kwa washindi walioshiriki katika shindano la uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari na makala kwa vyuo vya elimu ya juu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mashindano hayo yalihusisha washiriki kuandika insha na makala juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.

Akikabidhi vyeti na zawadi hizo kwa washindi mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano DK. Maria Sasabo amesema amehamasika kuona vijana wameshiriki katika mashindano hayo na kutoa maoni juu ya faida, changamoto na mbinu mbali mbali za kukabiliana na changamoto hizo katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.

Aidha, Dr. Sasabo ametoa rai kwa vijana kutumia fursa mbali mbali zitokanazo na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kukuza vipaji, kujielimisha na pia kupata ajira.Pia, amewaasa vijana kutumia huduma mbali mbali za mawasiliano kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kwa ustawi wa wao kielimu, kijamii na kiuchumi.
Regani Yudos kutoka shule ya Msingi Mbuyuni akipokea cheti na zawadi ya mshindi wa pili katika shindano la kuandika insha kwa shule za msingi
Jane Michael Andrew wa Mbuyuni mshindi wa kwanza katika shindano la kuandika insha kwa shule za msingi akipokea cheti na zawadi kutoka kwa mgeni.
Felician Crispin Kapama kutoka Zanaki Sekondari mshindi wa pili shindano la kuandika insha kwa shule za sekondari.
Omary Abas Mdungu mshindi wa kwanza makala kwa vyuo vya elimu ya juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera washindi, muendelee kufanya vizuri shuleni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...