Na Ally Daud-Maelezo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama anatarajia kuzindua rasmi Taasisi yenye jukumu la kuboresha ubunifu na ushindani wa kibiashara katika sekta binafsi (TEEC).

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji TECC, Bw. Sosthenes Sambua amesema kwamba sambamba na uzinduzi huo, leo taasisi hiyo itaendesha kliniki ya biashara katika viwanja vya Mlimani City leo.

“Mbali na Uzinduzi wa TEEC leo kutakuwa na maonesho ya wajasiriamali katika viwanja hivyo na kutakuwa na kliniki ya biashara kutoka kwa taasisi 15 zitakazotoa ushauri na ujuzi kwa vijana wanaotaka kujiajili bila malipo siku nzima” alisema Bw. Sambua.

Aidha Bw. Sambua amesema kuwa TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha biashara zinazoongeza thamani kwa mazao ya Tanzania na kutengeneza bidhaa kwa maendeleo ya nchi.

Mbali na hayo Bw. Sambua alisema kliniki hiyo itakuwa ni fursa ya kukutana na wataalamu kwenye nyanja za ujuzi, mitaji, kodi, usajili, leseni, viwango, mitandao ya biashara na malezi miongoni mwa wataalamu wengine.

Taasisi hii imeundwa kwa pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa alisema ushirikiano wa COSTECH na TPSF katika kuunda TECC unaendana na sera ya baraza hilo linalotaka kuona watanzania wanamiliki sehemu kubwa ya uchumi wao kwa kuwafanya kuwa washiriki. 

“Tunatambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati ili waweze kuzalisha bidhaa na kutoa huduma bora, kuwa washindani kimataifa ili kufikia dira ya taifa ya maendeleo 2025,” alisema Bi. Issa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi leo ili kufaidika na kliniki hiyo ya biashara kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi kwa jamii na Tanzania kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...