Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiongea na Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam wakati akiwatakia heri katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Arusha.
 Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwapa mkono wa heri Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam kuelekea katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayatarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Jijini Arusha. 
 Wapiga golf wa Klabu ya Lugalo wakifanya mazoezi ya Mwisho  kabla ya kuondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam kuelekea katika  mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayotarajiwa kufanyika hivi Karibuni Mkoani Kilimanjaro na Arusha.

Na Selemani Semunyu,JWTZ
Timu ya golf ya Jeshi ya Lugalo imetakiwa kuhakikisha inawapa raha wanachama wake akiwemo  Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi Open mashindano yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiongea na Wachezaji hao katika mazoezi yao ya Mwisho katika Klabu ya Lugalo Jijini  Dar es Salaam  kabla ya Kuondoka kuelekea Moshi.

"Hakuna sababu kwa Timu ya Jeshi iliyofanya mazoezi kwa muda  Mrefu ikashindwa kirahisi katika Mashindano kama haya ambayo tuliwahi kuchukua ubingwa kiukweli wapeni raha wanachama wenu" Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.

Aliongeza kuwa Wanachama wa Lugalo akiwemo Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara hawahitaji kitu kingine zaidi ya Furaha ya Ushindi ambayo watakuwa wanaifuatilia hivyo ni Jukumu la wachezaji hao kuhakikisha wanakamilisha Furaha hiyo.

Pia aliwataka wanachama wa Golf kuhakikisha wanamtuma kazi ili kuhakikisha mafaninio makubwa yanapatikana ikiwemo kuboresha Uwanja wa Golf wa Lugalo ambao ni Uwanja uliojengwa na wazalendo kuwa Bora na kuhamasisha Mashindano mengi ya Kimataifa kuandaliwa katika Uwanja huo.

Mwenyekiti huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni aliahidi kuboresha Klabu hiyo na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi na Kuwa kiwanja bora Afrika Mashariki na kuwataka watu wote kujitokeza kushiriki katika mchezo huo kwani ni mchezo unaokubalika kwa rika zote.

Kwa upande wake Kapteni wa Timu hiyo Kapten Kassim Usitambe alisema Mara baada ya Mashindano hayo watakayoshiriki wakiwa ni wachezaji Tisa kutoka klabu ya Lugalo wataelekea Mkoani Arusha kwa mashindano ya Tanzania Open.

Kwa upande wake mmoja wa wapiga Gofu hao Amina Hamisi aliahidi kurejea na ushindi katioka mashindano hayo ili kutoa zawadio kwa mwenyekiti mpya ikiwa ni siku chache tu baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo.

Timu hiyo ya Golf iliyoondoka leo (Agosti Nne) itashiriki Mashindano hayo ya Moshi Open ambayo Klabu hiyo Mwaka 2014 walichukua kikombe yatashirikisha Wachezaji wote wakiwemo wa Nje sambamba na ya Tanzania open ambayo wapiga Gofu kutoka Nje ya Tanzania.     

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...