Na Selemani Semunyu, JWTZ.

Timu ya mpira wa Mikono ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imefanikiwa kurejesha nguvu yake baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Uganda  UPDF kwa 24-23 katika Mchezo wa Pili wa Timu hiyo uliokuwa na ushindani mkali baina ya Timu hizo.

JWTZ imeifunga UPDF Timu zote zilianza Mchezo taratibu huku wakijaribu kusomana wachezaji wa timu hizo hali il;iyokuwa ikibadioli mchezo huo katika kila dakika inayomalizika huku tanzani awakionekana kuwazidi wenzao wa Uganda.

Hadi Nusu ya Kwanza ya Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro ilimalizika huku Timu ya Tanzani ilikuwa ikiongoza kwa magoli 12 -9 dhidi ya Uganda ambao walionekana kupoteana katika kipindi hicho chwa kwanza.
Mchezaji wa Timu ya Tanzania Mtumwa JUma akipambana na walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23.

Kipindi cha pili Uganda waliingia kwa Nguvu huku wakionyesha kufaidika na Kipindi cha mapunziko kwani walifanikiwa kupunguza idadi ya Tofauti ya magoli na kuibana Tanzania kutokuwa na tofauti kubwa na hatimaye kufanikiwa kutoka uwanjani wakiwa wamefungana kwa tofauti ya Goli Moja.

Nahodha wa Timu ya Tanzania  Sedrick Damiano alisema kipingon walichopata katika Mchezo wa kwanza kutoka kwa Rwanda kimewafanya kubadilika na kurekebisha makosa yaliyojitopkeza sambamba kuwa makini na Waamuzi.

Pia Alisema ni mategemeo yake ushindi huu utakuwa salamu tosha kwa Wapinzani wao Kenya ambao watakutana nao katika mchezo unaotarajiwa kufanyika Agosti 14 katika uwanja wa Amahoro.

Kwa Upande wake mkurugenzi  wa Michezo wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu alisema ushindi huo umewapa nguvu ya kuhakikisha wanashinda katika michezo iliyosalia.

Katika Mchezo Mwingine katika Mpira wa pete Tanzania inatarajiwa kukutana na Wenyeji Rwanda wakati katika Mpira wa Miguu Tanzania inatarajia Kukutana na Kenya katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania Ally Hamisi (Mwenye jezi namba 11) akipambana na walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23.
Mshambuiliaji wa Timu ya Tanzania Ally Hamisi (Mwenye Mpira ) akitafuta namna ya kuwatoka walinzi wa Timu ya Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23.
Baadhi ya mashabiki wa Timu ya Tanzania Wakishangilia wakati Timu yao ikipambana na Uganda wakati wa michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki kat.ika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo Tanzania ilishinda 24-23.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...