Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imekusanya sh.Trioni 1.055 kwa mwezi julai sawa na asilimia 95.6 ya lengo la kukusanya sh.trioni 1.103 iliypangiwa na serikali kwa mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo amesema kuwa ukusanyaji huo huo umetokana na mwitikio kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kufanya kuongezeka kila mwezi.

Amesema kipindi cha mwezi Julai 2015 TRA ilikusanya sh. Bilioni 914 sawa na asilimia 15.43.

Kayombo amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 mamlaka hiyo imepewa lengo la kukusanyanya sh.Trioni 15.1 ikilinganishwa na lengo la kukusanya sh.Trioni 13 .32 ya mwaka wa fedha 2015/2016.

Amesema mikakati iliyopo kwa mamlaka hiyo kuhakikisha walipakodi wapya wanasajiliwa zaidi pamoja na kuhuisha taarifa za walipakodi kwa kuhakikisha namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) na ambazo hazitumiki zitafutwa katika mfumo wa TRA.

Kayombo amesema kuwa hadi sasa waliochukua mashine za kieletroniki EFD ni 2700 na wengine walikuwa wanazitaka mashine lakini wamekosa sifa.

Aidha amesema kuwa katika mkakati mwingine ni ukusanyaji wa mapato ya kodi za nyumba ambapo watatembea nyumba hadi nyumba na kutaka wapangaji kutoa ushirikiano.
 Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mampato Tanzania(TRA), Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa ukusanyaji huo huo umetokana na mwitikio kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kufanya kuongezeka kila mwezi.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Makao Mamkuu, Gabriel Mwangozi akifafanua jambo kuhusina na namna Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) walivyojizatiti katika mpango wa kutembea nyumba zenye wapangaji kwaajili ya kuwahamasisha kulipa kodi katika Mamlaka hiyo kwa kila mkoa hapa nchini. Kushoto ni Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru.
 Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mampato Tanzania(TRA), Richard Kayombo(Mbele) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera kwa kukusanya kodi. Lakini sidhani kama kufungia watu maduka yao ni suluhisho. Lazima kuwashawishi na kuwapa muda. Hawa watu wakifirisika huko mbele kiwango cha kukusanya kodi kitapungua. Tuwasimamie walipe kodi lakini tusiwaruhusu wakafirisika. Tumejifunza nchi za Marekani na Ulaya zikilazimika kutoa fedha ili kukwamua uchumi wao uliodorora. Hata China ilifanya hivyo hivyo. Sisi tusiruhusu wafanya biashara wakafirisika. Tuwabane. Tuwape muda. Tuwaelimishe. Tuwashawishi wajiandikishe, ili mtaji ubaki unazunguka. Hatimaye wataingia kwenye mfumo wa kulipa kodi. Tujifunze Marekani, Ulaya na China. Walitoa Stimulus Economy kwa wananchi wao ili biashara isidolore. Tuwasaidie wafanya biashara wasifirisike. Hili litalinda uchumi wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...