THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Tundu Lissu Mikononi mwa polisi, huenda akapandishwa kizimbani kesho

Na Mwene Saidi
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi na kwamba mapema kesho anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na Blogu ya Jamii kwa njia ya simu ,Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alisema mteja wake alikamatwa jana mkoani Singida.
"Alikamatwa jana saa 12 jioni mkoani Singida wakaanza safari akiwa chini ya ulinzi hadi Kituo cha Polisi Chamwino Mkoani Dodoma

"Leo mchana waliwasili Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam...walianza kumhoji saa 9 hadi 9;30 Mahojiano yalihusu kujihusisha na matamshi ya uchochezi katika viwanja vya mahakama ya Kisutu" alisema Kibatala.

Aidha alisema kwa mujibu wa sheria hadi kufika kesho asubhi Lissu atakuwa amekaa chini ya ulinzi wa polisi kwa masaa 36 kwa hiyo inatakiwa apelekwe mahakamani ama kuachiwa kwa dhamana.