Mkurugenzi wa Mtandao wa Shirika linalo andaa mashindano ya Dance Duniani (UDO),Ashraf Rwabigimbo akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kundi la washindi wa shindano la dansi (Dance Battle Zone) kwa mkoa wa Dar Es Dalaam,lililojulikana kwa jina la BITZ, lililokuwa na washriki wawili ambao ni Amani Hamis na Beston Shaban kulia ni MKurugenzi wa fedha wa UDO East Africa,Bwa.Idris SD

Mkurugenzi wa Mtandao wa Shirika linalo andaa mashindano ya Dance Duniani (UDO),Ashraf Rwabigimbo akionesha medali walizozawadiwa washindi hao wa dansi.



Mkurugenzi wa Mtandao wa Shirika linalo andaa mashindano ya Dance Duniani (UDO),Ashraf Rwabigimbo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo,kuhusiana na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la dansi lililojulikana kwa jina la Dance Battle Zone kwa mkoa wa Dar Es Dalaam.Pichani shoto ni mmoja wa washindi Amani Hamis kutoka kundi la BITZ ambao walizwadiwa hundi ya shilingi milioni moja.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Shirika linalo andaa mashindano ya Dance Duniani (UDO),Ashraf Rwabigimbo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo,kuhusiana na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la dansi lililojulikana kwa jina la Dance Battle Zone kwa mkoa wa Dar Es Dalaam.

Ashraf alisema kuwa shindano hilo linawahusisha vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,na linafanyika kwa awamu mbili,na kwa upande wa Tanzania litafanyika katika awamu mbili ya mkoa na awamu ya pili itakuwa ni ya Kitaifa,ambalo litashirikisha jumla ya mikoa minne kwa kuanzia.Amesema kuwa shindano hilo limeanzia mkoa wa Dar Es Salaam,ambapo shindano hilo lilizinduliwa rasmi na Mbunge wa jimbo la Mikumi,Mh Joesph Haul a.k.a Prof Jay mnamo Agosti 2016 na kumalizika Agosti 28,ambapo kundi BITZ liliibuka mshindi na kuzawadiwa fedha taslim shilingi milioni moja.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Nadzz Lilbeast (Nadeem Nizar),mshindi wa tatu ni Tafa Makuzi,mshindi wa wanne ni Editoo Kinywele (Idris Hamza) ma mshindi wa tano ni Angel's (Angel Nyigu na Abdully Ally),washindi wote walikuwa wanawakilisha jiji la Dar .

Amesema kuwa baada ya Dar,mashindano hayo yatahamia mkoani Dodoma mwezi Septemba,ikifuatiwa mkoa wa Arusha mwezi Oktoba na Zanzibar kufanyika December 2016.Akaongesema kusema kuwa lengo la shindano ni kupata mshindi atakaewakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya UDO World Street Dance Championships,yatakayofanyika huko Glasgow Scotland,mwakani Agosti 2017.

Washindi wa shindano la dansi ( (Dance Battle Zone) kwa mkoa wa Dar Es Dalaam Amani Hamis na Beston Shaban wakionesha umahiri wao wa kucheza kama sehemu ya kionjo,ndani ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.PICHA NA MICHUZI JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...