Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) yanayopangwa  kufanyika Septemba 1 mwaka huu. Maandamano hayo  yamepewa jina la UKUTA ambapo wanachama wake wanataka kuingia mitaani kupinga kile wanachokiita ukandamizaji wa demokrasia.
 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema leo kwamba maandamano hayo hayatafanyika na jeshi la polisi limejipanga kuzuia maandamano hayo.
Kamanda Sirro amesema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayedhubutu kuingia barabarani kutokana jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.
Amesema kuwa utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa hivyo kufanya mikutano bila kufuata utaratibu hautaruhusiwa.
Kamishina Sirro amesema kuwa kikundi/watu  wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja Amani kwa Dar es Salaam hakuna kitu chochote kitafanyika kutokana na jeshi la polisi lilivyojipanga.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Agasti 20 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye  maneno ‘UKUTA’ fulana 6  za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’. 
Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Yoram Sethy Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani. 
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya Operesheni mbalimbali za kanda hiyo pamoja na kuzuia maandamano ya UKUTA, jijini Dar es Salaam leo.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine ya kuwekea risasi zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akioyesha bastola aina ya Browning yenye  risasi sita iliyokamatwa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha flana rangi mbalimbali zilizokamatwa. 
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...