Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega amewaondoa hofu wananchi wake na kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi kwani Rais Dkt. John Magufuli anania njema na watanzania.

Ulega ametoa kauli hiyo katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Sotele kilichopo kata ya Dondo wilayani Mkuranga.

Amesema kuwa hakuna haja ya kumchukia raia kwani anayoyafanya rais leo yamesababishwa na watu wachache ambao Kazi yao ilikuwa ni kujijali wenyewe tu na si vinginevyo. "Mnajuwa rais anadhamira ya dhati kabisa na watanzania na hasa katika bajeti ya mwaka huu ndio. maana fedha nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi hivyo kinachotakiwa nikumuunga mkono na kuzidi kumuombea tu." amesema Ulega

Akizungumzia maendeleo ya jimbo la Mkuranga alisema amejipanga kikamilifu kuwaletea maendeleo wananchi wake na ndio maana anapita kuwashukuru na kuhimiza maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibewa kilichopo kata ya Dondo, ambapo katika mkutano huo aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kisha akatumia fursa hiyo kusikiliza kero zao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Juma Abed akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Kibewa ambao aliwataka kumtumia Mbunge wao Ulega na kwamba ni muda wao sasa kumbebesha majukumu yao kwani ndio kazi waliyompa.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Kibewa Kata ya Dondo wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega (hayupo pichani).
Mbunge Abdallah Ulega wa Jimbo la Mkuranga akiwa sambamba na watendaji na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo akikagua mradi wa ufugaji wa samaki unaondeshwa na kikundi cha ufugaji samaki katika kijiji cha kibewa.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akimsikiliza Mganga wa Zahaniti ya Kijiji cha Sotele, Emily Bugingo wakati alipoitembelea katika kata ya Dondo bara, Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani. (Picha na Emmanuel Massaka,Globuya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. tuhamasishe uboreshaji wa makazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...