Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH, Dk Victor Ngotta (kushoto) akimfanyia upasuaji Eliudi leo kwa kushirikiana na Profesa Saber Waheeb (katikati) na Dk Mohamed Malak kutoka Misri (kulia).
  Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary akizungumza jambo baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana aliyekuwa na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo Leo.
 Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo akiwa ofisini baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana ambaye alikuwa na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo Leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Na John Stephen
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Leo imefanikisha kuwafanyia upasuaji watoto pacha ambao walikuwa wana tatizo katika njia mkojo.

Watoto hao wametoka katika chumba cha upasuaji salama na sasa wanaendelea vizuri baada ya kurejeshwa wodini. Watoto hao ni Eliudi Joel na Elikana Joel ambao wana umri wa miaka mitatu kila mmoja.

Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary na Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo wamefanikisha upasuaji wa Elikana wakati Eliudi amefanyiwa upasuaji na Profesa Saber Waheeb na Dk Mohamed Malak kutoka Misri kwa kushirikiana na Dk Victor Ngotta na Dk Mwajabu Mbaga wa Muhimbili.

Dk Bokhary amesema kuwa upasuaji wa watoto hao umechukua saa moja na nusu na kwamba hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya shughuli hiyo.

“Watoto hawa wataendelea kuwapo wodini hadi watakapopona vizuri ndio tutawaruhusu,” amesema Dk Bokhary.

Dk Bokhary amesema kuwa watoto wengine wawili leo wamefanyiwa upasuaji ambao walikuwa na tatizo kama hilo.

Jana madaktari wa hospitali hiyo walianza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakul

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Endelea kuboresha huduma.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana madaktari wetu. Nchi inasonga mbele. Sasa taifa letu litakuwa taifa kubwa na mataifa mengine yataleta wagonjwa wao hapa Tanzania. Nashangaa watu wanazidi kuandika mambo ya UKUTA kwa habari za mbele na habari muhimu kama hizi zikiwekwa kwenye kurasa za ndani. Waandishi si wazalendo. Wanashabikia siasa. Tanzania tumechoka na maneno sasa tunataka kazi kwanza. Watu wanachochea UKUTA mbona sijasikia wakiwapongeza Madaktari hawa. Tuache siasa uchwara. Taifa linasimama. Mungu awape nguvu madaktari hawa. Tunawapenda sana na kuwaheshimu kwa kazi zenu. Wana siasa hawana habari na ninyi wao wanajari siasa zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...