Asubuhi ya kuamkia leo huko Rio De Janeiro nchini Brazil katika michuano ya Olympic, mwanariadha Mjamaica Usain Bolt ameweza kupata ushindi tena wa pekee kwa kujipatia medali ya dhahabu kwa kukimbia mbio za mita 100 kwa sekunde 9.81.
Bolt ameweza kumpiku mpinzani wake Justin Gatlin mwenye asili ya America ambaye yeye amekimbia kwa sekunde 9.89 na kunyakua  medali ya Silver na mshindi wa tatu Andre de Grasse mwenye asili ya Canada akikimbia kwa sekunde 9.91.
Akiwa amejizatiti kuendelea kuweka rekodi, Bolt amebakisha michezo miwili ya mwisho ambayo atakimbia siku ya jumapili na kuweza kumaliza mashindano yake ya Olympic mwaka 2016
Mwaka 2012 katika michuano ya Olympic iliyofanyika nchini London katika mbio za Mita 100 na Mita 200 aliweza kushinda zote na kuondoka na Medali za dhahabu na Olympic ya mwaka 2008 iliyofanyika Beijing katika mfululizo huo huo wa mbio za mita 100 na 200 alifanikiwa kuchukua tena medali ya dhahabu.
Mkimbiza upepo huyo tangu aanze kushiriki Michuano ya Olympic mwaka 2008 hajawahi kushinda medali tofauti na dhahabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamaa anatimua mbio za mita mia moja na mita mia mbili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...