TBC inakuletea kipindi kipya maalum ambacho kitawakutanisha wadau mbalimbali wakijadiliana na kuongelea umuhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma, kama ilivyoagizwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli.
Kutana na Marin Hassan Marin katika kipindi hiki, kitakachoanza Jumatano, tarehe 10 August 2016 na kuendelea kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku TBC1, akikukutanisha watu mbalimbali katika kuchambua uamuzi huu muhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma.
Kutakuwa na maswali mbalimbali ambayo watazamaji watashiriki kuyajibu, na mshindi atajipatia zawadi kem kem.
Na tunaoishi nje tutawewza toa maoni yetu??
ReplyDeleteumeshasema unaishi nje, vipi wewe!
ReplyDeleteNadhani nlivyomuelewa mie mdau wa mwanzo hapo juu, itakuwa kakusudia japokuwa kuna waliyopo nje na ikatokea wana access ya kuki view hicho kipindi, je, na wao katika utoaji ama uchangiaji wa maoni yao juu ya mada husika, iwe kwa njia moja ama nyingine, wanaweza kuruhusika kufanya hivyo au kuna exclussive yeyote kwa waliyopo nje? Ila kama na mie ntakuwa sijakuelewa vizuri basi utaniwia radhi mdau uliyeuliza suali hilo hapo juu.
ReplyDeleteUnaweza kutoa maoni kwenye namba za WhatsApp 0678 279 107, au sms unaandika neno DODOMA unaacha nafasi kisha andika maoni au ujumbe wako, halafu unatuma kwenda namba 15559
ReplyDelete