TBC inakuletea kipindi kipya maalum ambacho kitawakutanisha wadau mbalimbali wakijadiliana na kuongelea umuhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma, kama ilivyoagizwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli.

Kutana na Marin Hassan Marin katika kipindi hiki, kitakachoanza Jumatano, tarehe 10 August 2016 na kuendelea kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku TBC1, akikukutanisha watu mbalimbali katika kuchambua uamuzi huu muhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma.

Kutakuwa na maswali mbalimbali ambayo watazamaji watashiriki kuyajibu, na mshindi atajipatia zawadi kem kem.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Na tunaoishi nje tutawewza toa maoni yetu??

    ReplyDelete
  2. umeshasema unaishi nje, vipi wewe!

    ReplyDelete
  3. Nadhani nlivyomuelewa mie mdau wa mwanzo hapo juu, itakuwa kakusudia japokuwa kuna waliyopo nje na ikatokea wana access ya kuki view hicho kipindi, je, na wao katika utoaji ama uchangiaji wa maoni yao juu ya mada husika, iwe kwa njia moja ama nyingine, wanaweza kuruhusika kufanya hivyo au kuna exclussive yeyote kwa waliyopo nje? Ila kama na mie ntakuwa sijakuelewa vizuri basi utaniwia radhi mdau uliyeuliza suali hilo hapo juu.

    ReplyDelete
  4. Unaweza kutoa maoni kwenye namba za WhatsApp 0678 279 107, au sms unaandika neno DODOMA unaacha nafasi kisha andika maoni au ujumbe wako, halafu unatuma kwenda namba 15559

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...