Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
UTASHI wa Kisiasa unahitajika katika kuboresha Huduma kamili za dharura za uzazi salama (CEnoNC) katika vituo vya afya vilivyopo hapa nchini ili kuepukana na vifo vitokanavyo na uzazi kati ya mama na mtoto.

Hata hivyo utashi huo umeanza pale Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangwalla alipo waagiza Waganga wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini  kuwa na vyumba vya upasuaji ‘theate’ zenye kufanya kazi ipasavyo kwenye vituo vyote vya afya kwenye maeneo yao ndani ya miezi 6.

Agizo hilo liliagizwa na Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kigwangwalla alipotembelea kituo cha afya cha Mwandoya kilichopo Meatu mkoani Simiyu kilichopo umbali wa kilometa 60 kutoka hospitali ya wilaya ya meatu mwishoni mwa wiki mkoani humo likichukuliwa kisiasa litafanikiwa kwa haraka zaidi ili kuepukana na vifo vitokanavyo na uzazi katika hospitali zetu.

Vilevile Rais Dkt. Magufuli  alipowasili jijini Dar es Salaam akitokea Mkoani Mwanza alisema kuwa wanawake waendelee kuzaa tuu kwa kuwa elimu bure watasoma kwanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne bure hivyo basi ili kuwa na kizazi chenye nguvu na chenye afya tuboreshe vituo vyote vya afya  ili kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi kwa watoto wachanga na akinamama wakati wa kujifungua.

Kuvuja Damu, Kifafa cha Mimba, maambukizi baada ya kujifungua, kutoka kwa mimba pamoja na uchungu pingamizi husababisha vifo vya akimama na watoto wachanga kufariki dunia.
Ikiwa vyanzo vyote hivyo vya vifo vya akinamama na watoto wachanga huzuilika kwa kuwa na Upatikanaji wa huduma kamili za uzazi Salama (CEmoNC).  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...