THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIJANA WENYE UFAULU WA G.P.A YA 2.5 WANAWEZA KUSOMA VYUO VYA NJE KUTOKANA NA UFAULU HUO KUKUBALIKA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education, Abdumaliki Mollel amesema hayo leo jijini Dar, kuwa vyuo vya nje viko tayari kupokea vijana wenye sifa hizo.

Mollel amesema kuwa vijana wasikate tamaa Global Link Education iko kwa ajili ya yao katika kuhakikisha ndoto zao hazipotei kutokana na kukosa nafasi katika vyuo vya ndani

Amesema kuwa wazazi waache kuogopa gharama za kusoma vyuo vya nje kwani gharama za kusoma nje ni sawa na vyuo vya ndani hivyo vijana watumie furssa hizo.

Mollel amesema ndani ya nchi mwanafunzi anachukuliwa kujiunga na elimu ya juu kwa sifa kuanzia alama D sawa pointi 4 kama mfumo mpya wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na mfumo huo ndio utakaotuumika kwa mtu yeyote kwnda kusoma nje ya nchi

Amesema wazazi na wanafunzi wanachanganywa na mfumo huo na kutaka kuacha kutishika kutokana kuwa uwezo wao kusoma nje bado wanao.

Aidha amesema kuwa global link education inawaka vijana na wazazi kuchangamkia fursa zilizopo katika kusoma nje na mazingira ya vyuo hivyo vina uwezo naa ubora katika utoaji wa elimu katika fani mbalimbali.

Amesema kuwa wanafunzi kuwa kuna watu wamesoma masomo ya sayansi lakini kutokana vyuo vya udaktari kuwa vichache wanakosa nafasi hivyo wanashindwa kufurahi na masomo hayo ktika kuwaaletea matunda.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. HK Anasema:

    Ila 'background' ya hiyo picha somehow haijakaa vizuri, nadhani wapiga picha wetu hilo nalo ni la kuzingatia mana naamini tuna mazingira mazuri tu arround, ambayo unaweza kufanya timing na kupiga picha mithli ya hiyo na ikawa nzuri tu bila kuunda hoja au suali lolote kwa msomaji.