Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika, Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. 
Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...