Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akiomba dua  kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)jijini Dar es Salaam. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Dini.
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa Kanisa la Anglikana, Mchungaji John Solom(aliyeshika kipaza Sauti) akisali kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam. 
Katibu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), wakili Ramadhani Maleta (mwenye tai nyekundu) akitoa neno la Shukrani mara baada ya kumaliza ziara ya viongozi mbalimbali wa dini waliotembelea katika uwanja wa ndege unaoendelea kugengwa wa Terminal III jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), Mhandisi, Mohamed Millanga akitoa maelekezo kwa viongozi mbalimbali wa dini jijini Dar es Salaam leo walipotembelea na kuombea kiwanja cha ndege cha Terminal III kilichopo katika uwanja wa ndege wa Malimu Julius Nyerere (JNIA).
Picha na Yasir Adam, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunatumaini sasa wizara ya mali asili na utalii itatoka usingizini. Tumezoea kusikia sifa kede kede kuwa tuna vivutio vingi. Lakini cha ajabu zunguka Dar es Salaam nzima hakuna hata mabango yanayoonesha kuwa sasa unaingia kwenye nchi ya utalii. Hakuna sanamu za wanyama hakuna lolote. Mi nilitegemea kuona dalili za utalii katika miji yetu. Maneno ni mengi kuliko mikakati ya kuonesha vivutio. Biashara ni matangazo. Wekeni picha na sanamu za utalii kila kona ya nchi hii. Ili wageni wakishuka tu kwenye ndege wajue kweli wameingia kwenye nchi ya utalii. Mitaa iwekewe taa za kumulika usiku. Miji ipendeze na kuvutia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...