THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VITUO 34 VYA MRADI WA DART VYAUNGANISHWA NA MKONGO (fibre) WA TTCL

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura na Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare wametembelea mradi wa kuunganisha vituo ya Mabasi ya Mwendokasi (DART) kwenye mtandao wa mawasiliano wa TTCL kupitia njia ya Mkongo ili kiimarisha mifumo ya mawasiliano ndani ya vituo hivyo na DART na UDART.

Katika ziara hiyo iliwahusisha wadau wengine kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina,DART, UDART, TTCL, Wakala wa Serikali Mtandao pamoja na Maxmalipo walitembelea vituo vya Kivukoni, Posta ya zamani, Kagera na Jangwani

Akitoa tathimini ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha vituo hivyo, Meneja Mradi wa TTCL, Mhandisi Amossy Itozya amesema kuwa Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) imekamilisha kuunga jumla ya vituo 34 vya DART kwenye mtandao wa TTCL kwa kutumia Mkongo(Fibre)
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura na Mtenda Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare na wadau wengine wakiwa katika usafiri wa Mabasi ya mwendokasi.

“Vituo vilivyokamilika- 34, vituo vinavyofanyakazi kwa sasa kwa -27 na Vituo 7 viko kwenye hatua za mwisho za utekelezaji navyo ni; TipTop, Backresa, Kagera, Baruti, Corner na Kibo- muda wowote vitaanza kutoa huduma. Aidha kwa Kituo kimoja ambacho ni Posta ya zamani- Mkongo(fibre) bado hakijaungwanisha na Mkongo” amesema Itozya.

Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare amesema kuwa amefarijika na utekelezaji wa mradi, kwa vituo ambavyo vinafanya kazi tayari tumeishaanza kuona mabadiliko; utendaji wa vituo imeongezeka.

“Kwa kutumia Mkongo utasaidia kuondokana na changamoto ambazo zilikuwepo awali za kukatika mawasiliano na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa huduma ya usafiri. Kwa kutumia Mkongo(fibre) tunauhakika wa kuimarisha mifumo yetu ya ndani na kwenye vituo vya mwendokasi hivyo kuondoa usumbufu kwa wananchi katika kupata huduma” amesema Mhandisi Lwakatare.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura na Mtenda Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare na wadau wengine wakikagua njia zilizopitisha Mkongo wa TTCL.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu, Dr Kamugisha Kazaura alishukuru wadau wote waliosimamia mradi huu kwa kukamilisha, na kuahidi kuwa TTCL itafanya kazi na DART pamoja na wadau katika sekta ya usafirishaji bega kwa bega kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi na kwa wakati.

“TTCL ina uzoefu mkubwa katika kutoa huduma ya mawasiliano, tumeishaunga taasisi za serikali na binafsi ndani na nje ya Tanzania katika mtandao wetu. Hivyo, TTCL itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha DARTinafanikisha malengo yake kwa kutumia mtandao wa mawasiliano wa TTCL” Amesema Dr Kazaura
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura na Maafisa kutoka TTCL wakikagua kifaa katika kituo cha Mabasi ya Mwendokasi.