Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella(mwenye miwani)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa klabu mbalimbali wakati wa hafla ya ukabidhi vifaa kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Jijini Dar es Salaam leo.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akitoa neno la shukurani kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Hafla hiyo iliandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Vijana waliovyalia jezi za nyumbani na ugenini za timu ya Simba kwa msimu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara 2016/17 wakizinesha jezi hizo wakati wa hafla iliyoandaliwa na wadhamini wakuu ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali kwa timu zitakazoshiriki ligi hiyo.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura(kulia)

TIMU zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya shilingi milioni 514,208,400 /=.

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha  Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella ,alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.

“Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2016/2017”Alisema Mwiyombella.

Mwiyombella alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake  wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote,ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha  zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza  maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu  kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Mwiyombella.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru hiyo,  na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa mwito kwa klabu zote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.

Aliongeza kuwa  TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini  kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote  kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...