-Zaidi ya shilingi milioni 300 kushindaniwa
-Mshindi wa zawadi kubwa kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 100
Kampuni
ya Vodacom Tanzania
kwa kushiriana na benki ya CBA imezindua promosheni kubwa ambayo
itawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia fedha taslimu
kutoka kwenye kitita cha milioni 300 zilizotengwa kwa ajili ya
promosheni hii na mshindi mmoja wa zawadi kubwa atajishindia
kitita cha shilingi milioni 100.
Promosheni hii inayojulikana kama
‘Jiongeze na M-Pawa’ itatoa washindi wa siku wa shilingi milioni 1/-
kila mmoja,washindi wa wiki shilingi milioni 20/- kila mmoja na wateja
wapatao 200 wataongezewa mara mbili ya akiba zao
walizojiwekea kwenye akaunti zao za M-Pawa kila siku.
Promosheni
hii ambayo imeanza leo Agosti 31 itadumu kwa kipindi cha wiki 6 na
itafikia mwishoni mwezi Oktoba ambapo itafanyika droo ya kumpata
mshindi wa zawadi kubwa.Katika kipindi chote cha promosheni mabalozi wa
bidhaa za Vodacom na maofisa wa kampuni watatembelea sehemu mbalimbali
za Tanzania kwa ajili ya kuwaelimisha faida za kujiwekea akiba kupitia
huduma hii hususani wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ili
kushiriki kwenye promosheni anachotakiwa kufanya mteja ni kujiwekea
akiba kwenye akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha
promosheni.Kwa kujiwekea akiba mojamoja kutawawezesha wateja kujipatia
pointi za kuingia kwenye promosheni na kuwa na uwezekano wa kujishindia
fedha taslimu kila siku,kila wiki na zawadi kubwa ya promosheni.Kadri
mteja anavyojiwekea akiba kwenye akaunti yake
ya M-Pawa ndivyo anakuwa na nafasi kubwa ya kushinda .
Kwa
mfano kwa kujiwekea akiba kati ya shilingi 1,000/-mpaka 19,000/-mteja
anajipatia pointi 20,wakati akijiwekea akiba kati ya shilingi
20,000/-mpaka
shilingi 99,999/-mteja anajipatia pointi 40 na kadri anavyoweka akiba
ndivyo pointi zinaongezeka zaidi na kuwa katika nafasi nzuri ya
kushinda.
Kuweka
akiba kwenye akaunti ya M-Pawa na kuwa kwenye nafasi ya kushinda mteja
anaweza kupiga *150* 00# kisha kwenda kwenye menu ya M- Pawa,
chagua Weka kwenye M-pawa, weka kiasi cha fedha kisha weka namba yako
ya siri ya M-Pesa .
Wateja
watakaojishindia shilingi milioni 1/-na wale watakaoongezewa fedha
zaidi ya mara mbili ya akiba zao fedha zao zitaingizwa kwenye akaunti
zao za M-Pawa moja kwa moja ambapo watafahamishwa kuwa wameshinda
kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS).Washindi wa wiki wa shilingi
milioni 20/- na mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni watakabidhiwa
zawadi zao na maofisa wa Vodacom watakaochaguliwa kufanya
kazi hiyo kulingana na mikoa watakayotokea washindi.
Lengo
kubwa la promosheni hii ni kuwahamasisha watanzania kujenga utamaduni
wa kujiwekea akiba na kunufaika kwa mikopo yenye riba nafuu ya kati
ya asilimia 2% hadi 5% kulingana na akiba ya mteja aliyojiwekea.”Promosheni
inawakumbusha watanzania kuwa kuweka akiba kwenye M-Pawa ni chaguo la
busara hususani kwa wajasiriamali kwa kuwa inawezesha kupata mikopo
nafuu yenye riba ndogo”.amesema Ian
Ferrao,Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania .
“Huduma
ya M-Pawa ni akaunti ya benki kwenye ncha ya kidole chako ambayo
imebuniwa kuboresha maisha ya wateja!Zaidi ya watanzania milioni 4.8
wanaendelea kufurahia huduma hii na natoa wito kwa watanzania wengi
wajiunge zaidi na kufurahia huduma hii ya M-Pawa.Unavyojiwekea akiba
zaidi ndivyo kiwango cha kukopa kinavyoongezeka”.Alisisitiza Ferrao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...