Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja ,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwa kwenye mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Steven Mlote(hayupo pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini. 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.
Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile, vibali vya  usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...