Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Mwambusi (Pichani)amesema kuwa wachezaji wameweza kupata uzoefu na wamejifunza mbinu mbalimbali hasa kutokana na ukubwa wa michuano hiyo. Amesema hayo mara 
baada ya kuwasili nchini jana Usiku wakitokea kwenye mchezo wao wa Mwisho wa kombe la Shirikisho  barani Afrika  dhidi ya TP Mazembe.

Mwambusi amesema kuwa, wameweza kukutana na timu ambazo ni bora na nzuri na kuna mambo mengi ambayo wachezaji wamejifunza na wana imani watatumia fursa hiyo kuhakikisha wanatetea ubingwa wao msimu huu.

Amesema kuna vitu ambavyo tumejifunza kwenye mashindano haya na tunataka tuendelee kuangalia nguvu yetu inaishia wapi ili kusudi tujipange kama benchi la ufundi pamoja na wachezaji nini ambacho tumekipata kwenye mashindano haya na nini tutafute.

Akiongolea  kuhusiana na suala la nidhamu kwa wachezaji wake, Mwambusi amesema kuwa hilo wameliona na watalifanyia kazi kwani wachezaji muhimu waliweza kukosa mechi muhimu kutokana na kupatiwa kadi za njano.

“Wachezaji wamejifunza na wameshajua  kwenye mashindano mchezaji anatakiwa awe na   nidhamu ya namna gani, kwasababu wachezaji kadhaa ikiwemo Donald  Ngoma na Vicent Bossou wamekosa mechi zile muhimu kwasababu ya kadi za njano ambayo inaathiri timu kwasababu michezo ipo michache na wachezaji wanahitajika wote wawepo lakini amekosa kutokana na kadi.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni ajabu timu ambayo imedumu zaidi ya miaka 80 bado inatafuta uzoefu, na Azam watasemaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...