THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA SERIKALI KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA UHUSIANO


Mwenyekiti wa mkutano wa wadau wa Washirika wa Maendeleo Dkt. Donald Kaberuka akifafanua jambo kwa wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria mkutano wa kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mkutano unaojadili kuhusu namna ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB-Dkt. Donald Kaberuka (kushoto), akifafanua jambo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu, Jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile.

Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (kushoto) akisikiliza kwa makini hoja ya mjumbe wa Mkutano kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam

Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano wa Maendeleo nchini Tanzania, mkutano umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam.