NA VICTOR MASANGU, PWANI 

WAFANYAKAZI wametakiwa kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanachapa kazi kwa bidii bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo. 

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti mpya wa chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na afya (Tughe)Mkoa wa Pwani Catherine Katele,wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho ulioambatana na uchaguzi wa viongozi.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba wafanyakazi wa Mkoa wa Pwani wanapaswa pia kuachana na makundi ambayo hayana maslahi yoyote kwa taifa kwani serikali iliyopo madarakani haipo tayari kumvumilia mtumishi mzembe anayeshindwa kutimiza wajibu wake.

“Mimi kwanza napenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa kuweza kuniamini na kunichagua kuwa mwenyekiti wao mpya wa Tughe Mkoa wa Pwani, lakini kitu kikubwa nawaomba tuachane na kufanya kazi kwa mazoea hii ni hatari sana na kitu cha msingi ni kila mmoja wetu atekeleze majukumu yake ipasavyo,”alisema Catherine.

Katele,alisema kwamba katika uongozi wake atahakikishe anaweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwasaidia wafanyakazi kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuwapa moyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aidha aliongeza kuwa ataweza mpango kazi wake wa kupita katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwapa elimu wafanyakazi kuhusina na uwajibikaji pamoja na utawala bora.

Alisema,Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Magufuli haitaki kuona mtumishi au mfanyakazi yeyote analeta masihara katika utekelelzaji wa majukumu yao hivyo ni vema kuhakikisha wanajenga misingi imara katika kucha kazi na sio vinginevyo.

“Ni vema wafanyakazi sasa tubadili tabia zetu na tuendana na kasi ya Rais wetu, nadhani mnatambua serikali ya wamu ya tano haitaki kuona mtumishi ambaye ni mzembe kwa hivyo na sisi tujifunze ii kuepukana na kutumbuliwa,”alisema Mwenyekiti.

Katele,alisema anatambua kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wafanyakazi na wanachama wa Tughe kiujumla lakini kamwe wasitumie migomo na maandamano yasiyo na tija katika kudai haki zao ila ni vyema watu wakafuata utaratibu ulio sahihi.

Alisema,mara nyingi watu wanadhani kufanya migomo ndio suluhu ya kupata haki zao jambo ambalo sio sahihi na kwamba madhara ya kufanya hivyo ni makubwa kwani wanaweza kupoteza kazi bila sababu ya msingi.

Alisema ,kwasasa atatumia nafasi yake kushirikiana na wakuu wa idara ili kuona jinsi ambavyo wanaweza kuchukua hatua sahihi za kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki na maslahi yao kwa wakati.

Hatahivyo,Katele amewataka wafanyakazi kutii sheria za kazi huku akiwaomba watumishi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili waweze kusaidiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili.

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwenyekiti huyo mpya Catherine Katele alichaguliwa na kuwa mshindi baada ya kupata idadi ya kura 38.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...