Makundi mawili makubwa
ya kihalifu mtandao yanayo andika program hasidi “Malware” zenye mlengo ya
kudhuru mabenki yametangaza kuungana ambapo imezungumzwa kuwa huwenda ndio
sababu kuu ya kumepelekea takwimu mpya za mashambulizi dhidi ya taasisi za
kifedha kwa Mwezi (4, 2016 – 6, 2016) kuongezeka kwa Asilimia 16 (16%) kulinganisha
na takwimu za Mwezi (1, 2016 – 4, 2016) .
Makundi haya mawili
ambayo ni waandishi wa “Nymaim Trojan” pamoja na “Gozi
Trojan” katika hatua yao ya kuunganisha nguvu yanatabiriwa kuongeza
tishio kubwa la matukio ya wizi wa fedha katika taasisi za fedha duniani kote –
Na inatabiriwa makundi mengine yakielekea kufata njia hii ya kuunganisha nguvu
ili kuongeza kasi ya kudhuru na kuiba fedha katika Taasisi za fedha. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...