Baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwa inje ya Jengo la Makao Makuu ya Yanga.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUFUATIA tetesi za Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kutaka kujiengua pamoja na  kubadili msimamo wake wa kuikodi timu hiyo, wanachama wa klabu ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam wamempigia magoti na kumsihi asibadili maamuzi yake.

Wanachama hao wamemuomba Manji kutobadili msimamo wake leo katika kikao cha dharula kilichofanyika leo kwenye Makao Makuu ya timu hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Aidha wanachama hao wameikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuzungumza na vyombo vya habari pasipo kupata ridhaa ya chama.

Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam, Robert Lyungu Kasera ameutaka uongozi wa timu hiyo kuweka mkutano mkuu wa dharula ili kupitisha pendekezo lao la kumvua uanachama katibu wa Baraza la wazee Ibrahim Akilimali kwa madai kuwa kiongozi huyo anashirikiana na timu pinzani kukwamisha mpango wa Manji kuikodi timu.

“Huyu mzee ana mikakati ya  kuiharibu Yanga na hatufahi, haiwezekani aongee masuala ya Yanga pasipo ridhaa ya uongozi wa klabu na viongozi mfikishe taarifa hii kwa usahihi bila kumun'gunya na kikao hiki kinalaani kitendo alichofanya,” amesema Lyunga.

Katika hatua ya kujitetea Mzee Akilimali ameomba radhi na kuwataka wanachama wa Yanga wasifikirie  vibaya kwa kauli aliyoiongea kwani wao kama Baraza la Wazee wanamuhitaji sana Mwenyekiti wao Manji na ameweza kuisaidia timu yao kwa takribani miaka 10. "Labda niseme hivi Kama kukurupuka ni tusi kama nilivyomwambia Yusuf, basi naomba radhi kwake Manji na wanayanga wote”.

Kufuatia hilo Kaimu Katibu Mkuu Yanga amethibitisha kupokea pendekezo hilo ila amesema wao hawana uwezo wa kumfukuza mwanachama hadi mkutano mkuu ufanyike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hapo lengo la Manji limetimia

    ReplyDelete
  2. HUU wote unyonge!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...