EdithaKarlo wa blog ya jamii,Missenyi.

WANANCHI wa kijiji cha Bulembe Kata ya Minziro Wilaya ya Missenyi wamemtaka Mbunge wao kutatua changamoto walizonazo kijijini hapo.

Wananchi hao walimweleza mbunge wao Diodarus Kamala,Mbunge wa jimbo la Nkenge kuwa kijiji chao kina changamoto ya miundombinu ya barabara,shule na zahanati."Sisi huku hatujawahi kuona kiongozi yeyote wa serekali anakuja kututembelea yaani wewe Mbunge ndo kiongozi wa kwanza kufika hapa kijijini kwetu na umejionea mwenyewe changamoto zetu"alisema Beatus John mmoja wa wanakijiji

Alisema changamoto zilizopo kijijini hapo ni barabara kwani huwa wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 16 huku wakipita katikati ya hifadhi ya msitu wa minziro wenye wanyama wakali, kufuata huduma za kijamii kijiji cha jirani."Hapa wanafunzi nao hupata shida ya kutembea umbali mrefu kwebda shule,akitokea mgonjwa akitaka huwa ni shida,tunawabeba na kutembea nao kufuata huduma sababu hapa kijijini hatuna zahanati wala shule"alisema

Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dkt Diodorus Kamala akijibu changamoto za wakazi wa kijiji hicho amewahakikishia kuwa ataendelea kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili wanakijiji hao kwa kushirikiana nao.Kamala aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kuwatembelea wapiga kura wake jimboni kwake.

Alisema kijiji hicho kina changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara,afya na elimu na atafanya kazi kwa kushiriana na wananchi hao ili kuhakikisha changamoto hizo zinaisha.Alisema watendaji wengi hawafiki kijiji hapo kwaajili ya kutatua kero zao sababu ya miundombinu ya barabara,badala yake wengi wanaishia kijiji cha ng'ambo.

Akionyesha kukerwa na ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya watendaji Kamala alisema ataweka daftari la mahudhurio kijijini hapo."Nitaweka daftari la mahudhurio kwa mwenyekiti wa kijiji kila mtendaji wa serekali akifika huku asaini kitabu hicho na baada ya miezi sita nitarudi kuona hali ipoje,wasipofika wajiandae kushughulikiwa hii serekali ya sasa ni kazi tu"alisema

"Pamoja na sura za furaha ninazo wanaona nazo,mtu hawezi kuamini kama mnaishi na hizi changamoto zote hizi kwakweli nawapongeza sana kwa hili"alisema Kamala huku wananchi wakimshangiliaNaye Diwani wa kata ya Minziro Twaha Lubyai alisema watafanya kazi kwa kuenda na kasi ya serekali iliyopo madarakani kwa kutembelea mtaa kwa mtaa ili kujua kero za wananchi na kuziwekea mikakati ya kuzitatua.

Diwani huyo aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wao ili kuleta maendeleo katika kijiji chao.
Mbunge wa jimbo la Nkenge Deodarius Kamala akiongea na wananchi wa kijiji cha Bulembe kata Minziro wakati wa ziara yake kwenye mkutano wake wa hadhara wa kujua kero za wananchi .
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya missenyi Projestus Tegamaisho akiongea na wananchi wa kijiji cha Bulembi wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Nkenge
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bulembi na viongozi wa kijiji hicho wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nkenge katika mkutano wake wa hadhara kijijini hapo.
Akina mama wa kijiji cha Bulembi wakimkabidhi mbunge wao zawadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nikupongeze mbunge wetu, mimi mwenyewe sijawahi kufika huko japo ni mzaliwa wa Minziro nilikuwa nasikia habari za Burembe ila kwa kweli wanahitaji msaada maana ni mbali na huduma zote a kijamii. Hata diwani hajawahi kufika na si ajabu hata hakukuwa na kituo cha kupigia kula. Awamu ya tano tunaipongeza sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...