THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wateja wa Airtel kuongeza pesa kadi zao za usafiri wa mabasi ya mwendokasi kupitia huduma ya Airtel Money

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza huduma mpya itakayowawezesha wateja wake wa Airtel Money kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money 
 Mpango huu ni sehemu ya juhudu za Airtel kuendelea kutoa huduma za kibunifu zenye gharama nafuu zinazochochea urahisi na usalama katika kufanya malipo katika huduma za usafiri Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa amesema” Tunaamini kwa kuanzia mfumo huu wa kibunifu wa kieletronic katika kufanya malipo kutawahakikishia wakazi wa Dar es salaam usalama, urahisi na uharaka katika kufanya malipo ya huduma za usafiri, lengo letu ni kuhakikisha wateja wetu wananapata urahisi katika kufanya malipo yao mbalimbali ya kila siku ikiwemo kuongeza pesa katika kadi zao za mabasi ya mwendokasi ili kuboresha na kurahisisha safari zao ndani ya jiji”. 
 Tunaamini kuanzishwa kwa mfumo huu wa malipo kutaleta ufanisi katika huduma za usafiri na maisha ya jamii kwa ujumla kwakuwa kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwa wasafiri na kuwawezesha kulipia kadi zao kwa urahisi wakati wowote, mahali popote kupitia simu zao za mkononi “ aliongeza Naligingwa
 Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60#, kisha kuchagua 5 kufanya malipo , kisha kuchagua 3 Mwendokasi (DART) na kisha kuingiza kiasi cha pesa, kisha kuingiza reference namba and mwisho kuweka neno la siri kwaajili ya kufanya malipo na kisha mteja atapata ujumbe wa kuthibitisha malipo yake
 Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea wakati wakuitambulisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money, akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde

Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea wakati wakuitambulisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    hizo kadi zenyewe hazipatikani kila ukienda ukienda unaambiwa zimeagizwa!!