Na Mwandishi Wetu,
Zaidi ya watoto 50 leo wamehudhuria kambi tiba ya GSM Foundation inayoendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Mifupa na upasuaji ya MOI, yenye lengo la kupunguza vifo na mtindio wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, ambayo leo imeingia katika mkoa wa pili katika msimu wake wa pili pia, wenye lengo la kuwafanyia upasuaji watoto 100.

Kaimu Mkuu wa kambi hiyo iliyoanzia mkoani Mtwara Jumanne ya tarehe 2 mwezi huu, DK Shaaban Hamis, amesema, muiyikio walioupata katika mkoa huu ni muitikio mkubwa zaidi ukilinganisha na mkoa wa Mtwara, ambako ndio kunakosadikika kuwa na wagonjwa wengi zaidi, kutokana na rekodi waliyonayo, baada ya tafiti mbali mbali.

"Inawezekana hapa tukafanyia upasuaji wagonjwa hata 50 kwa siku hizi tatu tutakazokuwepo, na labda tukavuka lengo katika mikoa iliyobaki ya Iringa na Mbeya ambayo ndio ya mwisho katika msimu huu wa pili", alisema Dk Shaaban.

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Taasisi ya GSM ambayo kwa mwaka huu imewekeza zaidi kusaidia sekta ya Afya na Elimu amesema wanafarijika kuona wagonjwa wanakwenda kutibiwa kama walivyodhamiria, maana ndio lengo haswa, kusaidia kupunguza vifo vya watoto ambao wanasadikika kuzaliwa 4000, kwa mwaka lakini kati yao, ni asilimia 25 tu hurudi hospitalini kwa matibabu huku asilimia 75 wakishindwa kutokana na sababu za kiuchumi.

Tiba pekee kwa mtoto mwenye kichwa kikubwa, ama mgongo wazi ni upasuaji, tiba ambayo gharama zake ni kuanzia shilingi laki tatu za kitanzania, mpaka milioni moja, kulingana na ubora wa vifaa ama hospitali anayotibiwa mgonjwa.

Tanzania ina madaktari Bingwa tisa tu wenye uwezo wa kufanya upasuaji wa namna hii ambapo nane wanafanya kazi MOI na mmoja anafanya kazi katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza huku mikoa mingine yote ikiwa haina madaktari wa namna hii.
Wagonjwa wakisajiliwa katika chumba maalum cha kuwapokea katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma 
 ...kazi ya upasuaji ikiendelea maabara
Dk Shaaban Hamis, Naibu Mkuu wa Msafara akiwa kazini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...