THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA WATENDAJI KUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa wageni wake Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara haramu ya dawa za Kulevya kutoka Shirika la umoja wa mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu (UNODC) Bw. Johan Kruger (kulia), Mratibu wa kupambana na uhalifu wa majini Bi. Kaitlin Meredith (wa pili kulia) na mwingine ni mtendaji kutoka UNODC walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara haramu ya dawa za Kulevya kutoka Shirika la umoja wa mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu (UNODC). Bw. Johan Kruger (wa pili kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Wengine pichani ni watendaji kutoka Shirika la umoja la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba kutoka Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bi. Mercy Mrutu (wa kwanza kulia).