Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akizungumza na watendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Bi. Kaitlin Meredi (kulia) na Johan Kruger(kushoto), walipomtembelea ofisini kwake,jijini Dar es Salaam,leo. Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujadili njia muafaka za kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa jamii. 
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC),Johan Kruger(kushoto), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia juhudi mbalimbali za kupambana na biashara haramu ya Dawa za Kulevya.Kulia ni Mratibu wa Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith. 
Mratibu wa Programu ya Kupambana na Uhalifu wa Majini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Kaitlin Meredith (kulia), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, masuala yanayohusu udhibiti wa uhalifu unaofanyika majini walipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),akiagana na Mratibu wa Programu ya Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith, mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...