Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda.
Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa wa mchezo huo wa Gofu kutoka nchini Kenya,Jacob Okelo akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita,kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania ,yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya USA River na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Afisa Maendeleo ya jamii na Uhusiano,Justine Kesi ikiwa ni sehemu ya kiasi cha fedha kilichotolewa na Wadhamini waliodhamnini mashindano hayo ya Gofu kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya huduma za jamii mbalimbali kwa vijiji vinavyozunguka viwanja vya Kili Golf,jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River  jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...