WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekabidhiwa Uwanja wa Uhuru uliokuwa unakarabatiwa kwa takribani miaka mitatu.
Akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Elissante Ole Gabriel amekabidhiwa uwanja huo uliogharimu zaidi ya bilioni 12 uliojengwa na Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China.
Nape amesema kuwa, uwanja huu mbali na kutumika kwa ajili ya michezo anatoa fursa kwa vyama vya michezo kuja kufungua ofisi zao kwani kuna eneo kubwa sana ambaloliko wazi.
Uwanja huo kwa sasa una uwezo wa kuchukua mashabiki 25000 watakaokuwa wameketi tofauti na awali na ukarabati huo utaudumu kwa takribani miaka 200.
Uwanja wa Uhuru ulivyo karabatiwa na Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Elissante Ole Gabriel kulia akisaini baada ya kukabidhiwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. aliyekaa kushoto ni mwakailishi wa Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China wakisaini mikataba kabla ya kukabidiana uwanja huo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa uwanja wa Uhuru uliokuwa ukikarabatia na kampuni kutoka nchini China.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...