Lorietha Laurence - WHUSM

Michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuimarisha ushirikiano na mahusiano baina ya nchi na nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufunguzi wa michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) ambayo imeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa ni fahari kubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa kuwa inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kujumuika kwa pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimichezo.

“Kuunganisha nchi na nchi si kazi rahisi lakini kupitia michezo imekuwa ni jambo rahisi kwa kuwa inawafanya kuwa na umoja uliothabiti na hivyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi husika” alisema Mhe. Nnauye

Aidha Mhe. Nnauye aliwataka washiriki wasiishie kwenye michezo tu bali pia watumie fursa ya kuwepo nchini kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika Jijini la Dar es Salaam ikiwemo Makumbusho ya Taifa pamoja na Bagamoyo ambako kuna historia kubwa ya nchi.

Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ameeleza kuwa mashindano hayo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa yanawasiadia kuimarisha afya pamoja na kushirikiana katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

“kupitia michezo hii tunaimarisha afya pamoja na kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo walimu ikiwemo ukosefu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na namna ya kutatua tatizo hilo “ alisema Bw. Mukoba.

Kwa upande wake Rais wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda amesema kuwa kupitia michezo hiyo walimu hujifunza tamaduni mbalimbali baina yao ukizingatia elimu ndio msingi wa maendeleo.

Mashindano haya ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) yanafanyika kwa mara ya sita huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza ikihusisha nchi za Namibia, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika ya Kusini, Swizland na Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...